Loading...
 

Uundaji wa Klabu- Jinsi Tunavyoweza Kusaidia

 

 

Jamii ya Agora Speakers na Agora Speakers International wanaweza kukusaidia kuanzisha klabu kwa njia tofauti:

  • Kushauri na kutoa vidokezo kutoka watu ambao wamepitia njia hii, ikiwemo mapendekezo ya mahali pa mkutano.
  • Nyenzo za kielimu.
  • Kuwafunza mtandaoni wanachama
  • Vipindi vya maswali na majibu
  • Uendeshaji wa tovuti
  • Violezo, nembo, mabango, na vifaa vya kuandikia vyenye chapa.
  • Unaweza ukatengeneza nyenzo zote pale ulipo. Hamna haja ya kununua vitu kutoka sehemu moja kuu.
  • Usaidizi rasmi - tunaweza kutuma barua rasmi za kusaidia kwenye mamlaka zinazotakiwa ili kuthibitisha kuwa kazi au shughuli ni ya kielimu, sio ya faida, na inashirikiana na Shirika la duniani kote.
  • Matangazo ya kulengwa ya klabu au tukio lenu, kama hii ni klabu ya kwanza kwenye mji wako.

Hata hivyo, kumbuka kuwa klabu ni za kiambo, zinajitegemea zenyewe na zinaongozwa na maofisa wakujitolea wa kiambo ili kuwanufaisha wanachama wa kiambo. Kwahiyo, Agora Speakers International haiwezi kusaidia na:

  • Fedha
  • Bidhaa za bure za aina yoyote ile.
  • Utiifu wa sheria za kiambo.
  • Bima, kama inahitajika.
  • Kutafuta mahali pa mkutano au kujadiliana na wamiliki wa mahali pa mkutano wa kiambo.

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Monday May 31, 2021 14:31:36 CEST by zahra.ak.